Mwanamuziki wa Nigeria, Yemi Alade, amesema kwamba msanii anayetamani kufanya naye kolabo kutoka nchi za Afrika Mashariki, ni Ali Kiba kwa kuwa ana sauti na uwezo mkubwa wa kuimba.

Yemi Alade alitoa kauli hiyo katika kipindi  cha Sporah show alipoulizwa kuhusiana na msanii anayetamani kushirikiana naye kutoka Afrika Mashariki.

Mbali na  Afrika Mashariki Yemi Alade alisema anatamani kushirikiana na wasanii wenye majina makubwa katika muziki duniani akiwemo Nick Minaj anayempa kipaumbele namba moja akimuita malkia wa Ulaya na Afrika katika muziki. Wengine ni Beyonce, Riyana na Faly Ipupa anayefanya shughuli zakeza kimuziki nchini Ufaransa.

Prof. Mbarawa amteua Dk. Mgwatu kuwa Mtendaji Mkuu TEMESA
Mbowe: JPM Kagera unaenda lini?

Comments

comments