Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali jiji Dar es salaam.

Akitoa taarifa hiyo Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro ofisini kwake leo Septemba 16, 2016 amesema wakati kikosi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha kikiwa katika ufuatiliaji wa matukio ya wizi wa kutumia silaha katika maeneo ya Goba, Kawe Kinondoni, walifanikiwa kumkamata mwanamke mmoja  mkazi wa Goba ambaye baada ya kubanwa alitoa taarifa za majambazi wanaojihusisha na uvamizi wa maduka makubwa kisha mwanamke huyo alijaribu kutoroka Jeshi hilo. Tazama hapa video

Video: Hotuba ya Waziri mkuu Bungeni Dodoma, ahusisha mambo makuu 10
Wenyeji CECAFA Challenge Kupambana Na Kilimanjaro Queens

Comments

comments