Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM), umewaonya waliokuwa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, walioungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa), Edward Lowassa na Maalim Seif  kuwataka kuacha kutafuta huruma ya kisiasa.

Hayo yamesemwa na  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na vijana kutoka Jimbo la Dimani waliofiki ofisi kuu ya umoja huo kupokea namna ya kumnadi na kumwombea kura mgombea ubunge jimbo la Dimani.

Shaka amesema kuwa propaganda na uongo wa Maalim Seif, kwamba alishinda uchaguzi uliopita na anategemea kuapishwa na Umoja wa Mataifa umegota, na kuongeza kuwa alitegemea kusikia kutoka kwa Maalim akitangaza tarehe na mwezi atakaoapishwa.

“Lowassa na Maalim wanatambua hawakushinda Uchaguzi uliopita,wanachofanya nikuwachezesha kwata wafuasi wao na kuwapotezea muda, naamini Lowassa na mshirika wake hakuna mtakachobadilisha,”amesema Shaka.

Hata hivyo Shaka amesema kuwa hakuna kishindo chochote kitakachotokea kutoka kwa Maalim Seif na Lowassa hadi kuitikisa Zanzibar au Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwataka viongozi hao wakae kimya.

#HapoKale
Johnson: Hatujakurupuka kumfukuza Askofu Mokiwa

Comments

comments