Gianna Floyd mwenye umri wa miaka sita pekee, mtoto wa wa kike wa marehemu George Floyd ametoa ujumbe kuwa babayake amebadilisha ulimwengu.

Baba yake Floyd, alifariki wakati alipokamatwa na maafisa wa polisi wa Minneapolis wakati afisa mmoja alipomwekelea goti lake katika shingo yake kwa takribani dakika nane, huku kifo chake kikizua maandamano ya kupinga ubaguzi unaotekelezwa na polisi.

Matamshi hayo ya msichana Gianna yameonekana katika kanda ya video iliyochapishwa katika mtandao wa instagram, na Stephen Jackson, mchezaji wa zamani wa mchezo wa kikapu wa NBA na rafiki wa Floyd .

‘Babayangu alibadilisha ulimwengu’, alisikika akitabasamu na Jackson akaongezea , hiyo ni kweli , baba alibadilisha ulimwengu”.

Wakati wa mkutano na vyombo vya habari katika mji wa Minneapolis siku ya Jumanne, mamayake Gianna, Roxie Washington, alizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kifo cha Floyd alisema kwa uchungu kama mwanaye hana baba tena.

Katika taarifa fupi iliojaa hisia, alisisitiza kwamba mwanawe hana baba tena. hatomuona akikuwa ama hata kufuzu, hatoweza tena kuandamana naye wakati wa harusi yake.

Azam FC walilia nafasi za mabadiliko
Tottenham wakopa mabilioni kuikabili Covid-19