Klabu ya Tottenham inayoshiriki ligi kuu nchini England (EPL) imepata mkopo kutoka Benki Kuu ya England kiasi cha Pauni milioni 175 sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 511, Milioni 484, Laki 4, Elfu 11 na 375, fedha itakayotumika kupambania athari za janga la virusi vya Corona.

Spurs wamemesema watapata hasara ya kiasi cha hadi Pauni milioni 200 sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 584, Milioni 662, Laki 5 na elfu 12,000 kufikia Juni 2021, athari zinazojitokeza kutokana na michezo iliyosalia kuchezwa bila uwepo wa mashabiki na kulipa fidia kwa makampuni ya matangazo ya TV.

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alisema “tumekuwa na uendeshaji wa klabu hiyo kwa kuangalia uchumi zaidi hivyo lazima tujipatie fedha za kusaidia timu.”

Spurs, ambao wamecheza misimu minne mfululizo ya ligi ya mabingwa Ulaya hivi sasa wanakamata nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu nchini England ambapo pointi saba dhidi ya timu iliyonafasi ya nne Chelsea, mechi tisa zikiwa zimesalia.

Levy, ambaye alichukua nafasi ya Sir Alan Sugar katika nafasi ya Uenyekiti Februari 2001, aliongeza kwa kusema  ” Nilisema Marchi 18 kuwa katika miaka yangu 20 klabuni tumepitia changamoto nyingi lakini hakuna shida ambayo tumewai kupitia katika uongozi wangu inayofikia shida ya janga la virusi vya Corona (Covid-19).

Ujumbe wa mtoto wa Floyd "Baba yangu amebadilisha dunia"
Mkwasa afunguka ripoti ya vipimo

Comments

comments