Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (KJCI) imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kuiwezesha Taasisi hiyo kufanya upasuaji wa kihistoria tangu kuanzishwa kwake.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa Moyo Dkt. Bashir Nyangassa wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari bingwa wa moyo kutoka Hospitali ya Saifee ya Mumbai nchini India waliosaidia kufanikisha upasuaji huo wa kuvuna  mishipa ya damu mguuni na kupandikiza katika mishipa  ya moyo iliyoziba (CABG-Coronary Artery Bypass Graft) kwenye moyo .

Aidha, upasuaji huo uliwahusisha madaktari 6 toka Hospitali ya Saifee umesaidia kuwaongezea ujuzi wataalamu wa Taasisi hiyo na kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kuwasafirisha nje wagonjwa ili waweze kupata matibabu.

Akizungumzia upasuaji mwingine uliofanyika kwa wagonjwa 8 Dkt. Nyangassa amesema kuwa ni upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo ilikuwa na matatizo kwa kuibadilisha.

“Kwa upande wa upasuaji wa bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cath Lab tumetoa huduma mbalimbali za matibabu ya moyo bila kufungua kifua (catheterization) kwa wagonjwa 12 ambao tumezibua mishipa ya damu ambapo mgonjwa mmoja mshipa wake ulikuwa umeziba kwa asilimia 100,” Amesema Dkt. Nyangasa.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo  kutoka  Hospitali ya Saifee ya nchini India Dkt. Yunus Loya amesema kuwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete umeonyesha mafanikio makubwa na utakuwa wa kudumu.

Pia amesema kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wake wa nje ya nchi imefanya upasuaji bila kufungua na kufungua kifua kwa wagonjwa 79.

Hata hivyo, Mwaka 2016 Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohara Duniani Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal Saifuddin alifanya ziara yake hapa nchini na katika ziara hiyo kiongozi huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Dkt. John Magufuli na kumuahidi kuleta madaktari wa moyo. nchini watakaoshirikiana na Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na kufanya matibabu kwa wagonjwa

Waziri Mkuu wa Ethiopia kutua nchini kesho
Slaven Bilic Akalia Kuti Kavu