Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao hivi karibuni kuwa inawaandalia walimu sare maalum.

Taarifa hizo zilizosambaa kwa kiasi kikubwa kupitia whatsap zinadai kuwa Waziri wa wizara hiyo, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazokuwa wakivaa wakati wa kazi.

“Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza,” inasema sehemu ya tarifa rasmi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi iliyotolewa leo na kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Imeeleza kuwa Serikali itawachukulia hatua za kisheria wale towo waliohusika kuandaa na kusambaza habari hizo zisizo za kweli.

 

Manny Pacquiao Kupigana kwa Mara ya mwisho Marekani Wiki Hii
Mapenzi: Faida ya Kuvaa socks miguuni wakati wa tendo la ndoa