Klabu ya AC Milan ipo mbioni kufanya mazungumzo na kiungo kutoka nchini Hispania Santi Cazorla ambaye anakaribia kumaliza mkataba wake Emirates Stadium.

Arsenal wamekua kimya kuhusu mustakabali wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, jambo ambalo linaendelea kutoa mwanya wa klabu nyingine kama AC Milan kuanza kujisogeza na kufanya mazungumzo.

Mkataba wa Cazorla utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu na mara kadhaa amekua akionyesha kuwa tayari kufanya mazungumzo na uongozi wa Arsenal, lakini imekua tofauti.

Maafisa wa AC Milan Marco Fassone na Massimiliano Mirabelli wamelijumuisha jina la Cazorla kwenye orodha ya wachezaji watakaofanya nao mazungumzo katika kipindi cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo taarifa nyingine zinaeleza kuwa huenda mazungumzo hayo yakafanywa mwishoni mwa mwaka huu, ili kuangalia uwezekano wa kumsajili mwezi Januari mwaka 2017 kama Arsenal wataridhia.

Kwa sasa kiungo huyo yupo mjini Barcelona nchini Hispania, kwa ajili ya matibabu ya kisigino.

#HapoKale
Man Utd Kumbembeleza Zlatan Ibrahimovic