Hatimaye Ray C amerejea studio na Damian Soul kupika muziki aliouita ‘chakula kitamu’ kwa ajili ya mashabiki wake waliomkosa kwa miaka mingi.

Msanii huyo aliyewahi kubatizwa jina la ‘Kiuno bila Mfupa’ kutokana na uwezo wake wa kunengua, ameonekana katika picha akiwa studio za kisasa za Wanene Entertainment  pamoja na Damian Soul, akiwa amepungua mwili kwa kiasi kikubwa na kurejea umbo lake la miaka mingi iliyopita.

“God is good all the time…With my beautiful sister @rayc1982 in the kitchen cooking together with @salthak_tale ..something amazing is coming out,” Damian Soul ameandika kwenye picha hizo alizoweka Instagram.

ray-c-2

Hivi karibuni, Ray C amekuwa akipost kwenye Instagram vipande vya video vinavyomuonesha akiimba nyimbo zake maarufu za zamani, lengo likiwa kuwakumbusha mashabiki na kuwaaminisha kuwa bado sauti yake ina uwezo wa kufanya kitu kikubwa.

Makonda atangaza oparesheni mpya, aahidi Dar tulivu
Serikali Kupunguza gharama za mawasiliano

Comments

comments