Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera amesema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020, hakutakuwa na punguzo au nyongeza ya majimbo isipokuwa mbadiliko kwa baadhi ya majina.

Amesema NEC inatarajia kuwa na vituo 75,000 na kila kituo kitakuwa na watu 5 ambao ni Msimamizi wa Kituo atakayesaidiwa na Wasimamizi 2, Karani na Mlinzi.

“Tume mwaka huu haikuweza kuongeza majimbo, inabaki na majimbo 214 Bara na 50 Zanzibar na tunaenda kuyatangaza hivi karibuni majina ya majimbo hayo na Kata 3,956, hakuna mabadiliko. Mabadiliko yatakayotokea ni majina tu” Amebainisha Mahera.

Mkurugenzi huyo pia amesema Tume inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na inasubiri tangazo kwenye gazeti la Serikali la kuvunja Bunge ili itoe ratiba ya Uchaguzi.

Aidha, imeelezwa kuwa NEC inatarajia kutoa ajira zaidi ya 390,000 mwishoni mwa mwezi ujao.

Ambani ashtushwa na kipigo cha Simba SC
Wachezaji Simba SC kukabidhiwa Mamilioni