Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Septemba 18, 2016 amefungua muonekano mpya wa Bodaboda kwa kuwataka kufuata sheria na Wananchi kutambua kuwa hiyo ni ajira rasmi na si kazi ya kihuni kama ilivyozoeleka.

Uzinduzi huu umefanyika katika viwanja vya Leaders club na kuhudhuliwa na Wakuu wa Wilaya zote za jiji la Dar es salaam.

Aidha Kiongozi wa Bodaboda mkoa wa Dar es salaam, Daudi laurian amesema uzinduzi huo utawasaidia kutambulika popote pale walipo hivyo amewataka Bodaboda wote kutii sheria bila shuruti na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ubunifu wa wazo hilo

Video: Man United hoi mara tatu mfululizo
Waziri Nape atoa Motisha kwa wachezaji Serengeti Boys

Comments

comments