Mahakama jijini Barcelona nchini Hispania imemhumu kifungo cha miezi 21 jela mshambuliaji wa timu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi kwa makosa ya ufisadi wa kukwepa kodi.

Mchezaji huyo bora wa dunia pamoja na baba yake Jorge Messi wamekutwa na hatia ya makosa matatu yanayohusishwa na ukwepaji kodi katika uamuzi wa mahakama uliosomwa Jumatano hii.

Pamoja na kifungo hicho cha miezi 21 jela, Mahakama hiyo pia imewahukumu Messi na baba yake kulipa faini ya kiasi cha €2 milioni (Messi) na €1.5m (baba yake). Wawili hao wanadaiwa kufanya makosa hayo mwaka 2013.

Kadhalika baba yake amepewa kifungo cha jela kwa kufanya ufisadi wa kodi nchini Hispania kati ya mwaka 2007 na 2009.

Messi na Baba yake wakiwa Mahakamani

Messi na Baba yake wakiwa Mahakamani

Wawili hao pia wanakumbwa na faini nyingine ya mabilioni ya shilingi za kitanzania kwa kuficha fedha nchini Uruguay na Belize kwa lengo la kuzikwepesha kukatwa kodi (tax haven).

Hata hivyo, hakuna hata mmoja kati yao anayetarajiwa kwenda jela kwani kwa sheria za Hispania, kifungo cha chini ya miaka miwili jela kinaweza kugeuzwa kuwa kifungo cha nje kwa masharti ya kuwekwa chini ya kipindi cha uangalizi (probation). Pia, wameruhusiwa kukata rufaa katika Mahakama ya juu nchini humo.

Video: Mmarekani Mweusi alivyopigwa risasi sita kifuani na Polisi ‘Mzungu’
Audio: Kufuatia picha zinazosambaa kuhusu ajali ya Ngorika na Ratco Polisi Pwani wamezungumza haya