Pongezi kwa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara ya Kilimanjaro Queens zimeendelea kumiminika kwa kupokea salamu kutoka kwa watu, taasisi na mashirika mbalimbali baada ya kushinda Kombe la CECAFA Woman Challenge kwa kuifunga Kenya, goli 2-1.

Moja ya taasisi kubwa duniani ambayo imetuma salamu kwa Kilimanjaro Queens ni Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kwa kutuma ujumbe wa pongezi kwa Kilimanjaro Queens kupitia kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Salamu za FIFA zimetumwa kupitia ukurasa wa Twitter wa FIFA Women’s World Cup kwa kuandika “HISTORY! Congratulations Tanzania @Tanfootball, winning the inaugural CECAFA Women’s Championship, by beating Kenya 2-1. #KilimanjaroQueens”

Pamoja na pongezi hizo, pia Kilimanjaro Queens imepokea salamu kutoka kwa watu wengine akiwepo Waziri wa Michezo, Nape Nnauye, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na kocha wa timu ya taifa ya wanaume ya Uganda, Milutin Sredojevic Micho.

Drfa Yazipongeza Kilimanjaro Queens Na Serengeti Boys
Video: DC Sophia Mjema afungua kongamano la vijana Afrika Mashariki

Comments

comments