Wizara ya Elimu nchini Kenya imesema shule zote za msingi na sekondari nchini humo zitafunguliwa mwanzoni mwa mwaka 2021.

Wizara hiyo imesema shule hizo zitakapofunguliwa, wanafunzi wote wataendelea katika madarasa yao ya sasa.

Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Elimu, George Magoha amesema kwa mwaka huu hakutakuwa na mitihani ya kuhitimu itakayofanyika kwa shule za msingi na sekondari.

Kwa kawaida mitihani ya kumaliza shule nchini humo hufanyika kila mwezi Oktoba na Novemba.

Hata  Waziri huyo amesema vyuo na vyuo vikuu vinatarajiwa kufungua rasmi Septemba mwaka huu huku akisisitiza masharti yote ya kudhibiti maambukizi ya corona kuzingatiwa.

Jana, Jumatatu katika hotuba yake, Rais Uhuru Kenyatta aliamuru kufunguliwa kwa mipaka ya kaunti zilizowekwa kizuizini na kulegeza baadhi ya masharti huku akiipa Wizara ya Elimu saa 24 za muongozo kuhusu kalenda za kufungua shule.

Singida Utd kupambana hadi mwisho
Watakaoandamana "77 Nyeupe" kushughulikiwa

Comments

comments