Chama cha soka nchini England (FA) kimeifungulia mashataka klabu ya Hull City kwa kushindwa kuwatuliza wachezaji wake, wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Arsenal uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita jijini London.

Wachezaji wa The Tigers walimzunguuka na kumzonga mwamuzi Mark Clattenburg kwa shinikizo la kumtaka ampe adhabu kubwa beki wa pembeni wa Arsenal Kieran Gibbs, ambaye alimchezea ndivyo sivyo mshambuliaji wa pembeni Lazar Markovic.

Tukio hilo lilitokea wakati Hull city wakiwa nyuma bao moja kwa sifuri.

GK awakumbusha wasanii kurudi shule
#HapoKale

Comments

comments