Wamiliki wa mtandao wa Facebook wametangaza program maalum ya kuzishusha na kuzifungia picha zote za utupu kutoonekana kwenye mtandao huo, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji vilivyoakithiri katika siku za hivi karibuni.

Facebook wametangaza uamuzi huo leo baada ya watu kadhaa hususan wanawake kulalamika huku wengine wakiandamana wakipinga vitendo vya baadhi ya watu kusambaza kwa makusudi picha zao kwenye mtandao huo kwa lengo la kuwadhalilisha na kuwanyanyasa kisaikolojia. Vitendo hivyo vimebatizwa jina la ‘revenge porn’.

Kampuni hiyo imesema kuwa itaanza kutumia program ya ‘photo matching’ kuhakikisha kuwa picha zote zenye muonekano wa utupu na zilizolalamikiwa haziwezi kusambazwa kwa namna yoyote na kuzishusha kwenye mtandao huo.

“Kama mtu atajaribu kushea picha ambazo zimeshalalamikiwa na kuondolewa, tutamjulisha kuwa anavunja sheria na sera zetu na hivyo tumemzuia kuendelea na anachokifanya,” mkuu wa kitengo cha usalama cha Facebook, Antigone Davis anakaririwa na tovuti ya mtandao huo.

Utafiti uliofanywa umeonesha kuwa mtu mmoja kati ya watu 25 waliolalamika, wameeleza kuwa wameathirika au wametishiwa kuwa picha zao zenye maudhui ya utupu zitasambazwa kwenye mtandao huo.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 6, 2017
Video: Sirro awataka watuhumiwa wa dawa za kulevya kujisalimisha