Klabu ya AC Milan, ipo katika mipango ya kukifanyia marekebisho kikosi chake ambapo pamoja na mambo mengine inafanya mikakati ya kumrejesha mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang.

Aubameyang alitokea katika timu yao ya vijana kabla hajatimkia Saint Etienne ambapo alifanya vizuri na kupelekea kusajiliwa na Borussia Dortmund.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Dortmund Joachim Hand Watzke amesema Aubameyang hataondoka kirahisi kwani dau lake ni kubwa na sio chini ya pauni milioni 68.

AC Milan ingeweza kuwa inammiliki mchezaji huyo hadi sasa na inaujutia uamuzi wake wa kumuondoa mwishoni mwa mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 22, kwa kiasi kidogo cha fedha.

Mchezaji huyo aliwahi kuwa mfungaji bora akiwa na Milan, akifunga magoli matano kati ya michezo sita aliyoipiga. Lakini Le 10 Sports wanaripoti kuwa hakuweza kupewa nafasi kwenye timu kuu kutokana na ubaguzi wa kocha aliyewapendelea wachezaji wa Italia zaidi.

 

GSM wafungua duka Mlimani City
Uwanja Wa Namfua Waonesha Dalili za Mawingu Ya Mvua ya Ligi Kuu