Mashetani wekundu (Man utd) wameanza mazungumzo ya kutaka kumsajili tena mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic.

Zlatan aliitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa msimu uliopita, lakini mwishoni akakumbwa na majeraha na United kumweka kwenye orodha yay a wachezaji walioachwa.

Hata hivyo, pamoja na kwamba anatarajiwa kukaa nje hadi mwezi Januari mwakani, United wameanza tena mazugumzo ya kuhakikisha wanamsajili kwenye kikosi chao.

Awali taarifa zilisema kuwa anaweza kuondoka na kwenda kujiunga na moja ya klabu za nchini Marekani, lakini mwenyewe alikiri anataka kubaki kwenye Ligi Kuu ya England.

Ibrahimovic alifunga mabao 17 kwenye michezo 28 ya Ligi Kuu England msimu uliopita.

United wamesema kuwa watakuwa tayari kumsajili upya pale tu atakapokuwa amepona vizuri.

Mbappe Ampa Kazi Ya Ziada Florentino Perez
Shakespeare: Riyad Mahrez Kuikabili Arsenal Leo