Uongozi wa klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani umethibitisha kuachana na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, kwa kusema, hatoakua sehemu ya kikosi kwa msimu ujao wa ligi ya Merekani (MLS).

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 38, anaondoka mjini Los Angles, Marekani huku akiacha historia ya kupachika mabao 52, katika michezo 17 aliyocheza na kutoa pasi za mwisho 53.

Zlatan alijiunga na klabu hiyo maarufu duniani, mwezi Machi mwaka 2018 akitokea Manchester United ya England.

“Tunatoa taarifa kuwa, Zlatan hatoakua nasi kwa msimu ujao wa ligi ya MLS, tunamshukuru kwa mchango alioutoa klabuni hapa tangu alipojiunga nasi, tunamtakia kila la kheri katika maisha yake ya soka,” Alisema Rais wa LA Galaxy Chris Klein.

“Tangu mwaka 2018, Zlatan amekua msaada mkubwa katika kikosi chetu, ametoa mchango wa kutosha ambao umeisaidia klabu yetu kufikia malengo yake, japo kwa uchache. Tunajivunia kufanya kazi na mchezaji huyu, na tunaamini ipo siku atarejea hapa katika nafasi tofauti. Tunamshukuru sana Zlatan kwa kazi nzuri aliyoifanya.”

Taarifa za kuondoka rasmi LA Galaxy, zinaendelea kukoleza tetesi za mshambuliaji huyo kurejea barani Ulaya kujiunga na moja ya klabu nguli zinazotajwa kuiwania saini yake, kupitia dirisha dogo la usajili, litakalofunguliwa mwezi Januari 2020.

Kabla ya kujiunga na LA Galaxy, Zlatan aliwahi kuzitumikia klabu kubwa barani Ulaya kama FC Barcelona, Juventus, Paris St Germain, Inter Milan na AC Milan.

Wazimia baada ya fedha za kikoba kuyeyuka kwenye kibubu
Wizara, wanajeshi wastaafu kuimarisha sekta ya kilimo nchini

Comments

comments