Mbunge na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kuwa jukumu lake duniani ni kuiharibu CCM ili kukata mnyororo wa maendeleo duni nchini.

Hayo ameyasema wakati akijibizana na Mbunge Bashe kupitia mtandao huo wa Twitter.

Zitto ameandika hayo mara baada ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, (CUF) Julius Mtatiro  kung’atuka katika nafasi aliyokuwa nayo katika chama hicho na kutangaza rasmi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli.

”Wajibu nimejipa duniani ni ku destroy CCM ili kukata mnyororo wa underdevelopment nchini kwetu. Nikishindwa mimi watafanya kizazi kijacho Lakini CCM itatoka tu. Hakuna marefu yasiyo na ncha”

Aidha Bashe amemjibu Zitto Kabwe kwa kumwambia mabadiliko yanaweza kupatikana ndani ya CCM na si vinginevyo na kumtaka Zitto kuhamia CCM kama ambavyo viongozi wengine wanavyohamia.

”Kaka na Ndg yangu@zittokabwe, karibu CCM” ameandika Bashe kupitia Twitter.

Hata hivyo Zitto amemjibu Mhe. Bashe kuwa watasubiri sana.

Jeshi la Polisi latoa onyo kali kwa wanasiasa kuhusu uchaguzi
Video: Siasa za Maendeleo za CCM zamng'oa Mtatiro (CUF)

Comments

comments