Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amerusha makombora kwa pande mbili shindani zaidi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, CCM na vyama vinavyounda Ukawa kuwa sehemu ya ubadhilifu wa fedha za umma kwa nyakati tofauti.

Akizungumza jana katika uzinduzi wa kampeni za chama chake zilizofanyika katika viwanja vya Zakheim Mbagala, Dar es Salaam, Zitto alisema kuwa kuna ufisadi unaoendelea serikalini kupitia bandari ya Dar es Salaam ambapo baadhi ya mizigo huingia nchini bila kulipa kodi kwa madai kuwa inapita kwenda nchi za jirani lakini huichia nchini.

Zitto aliongeza kuwa wakati mchakato wa uchaguzi unaendelea, bado watu wachache wameendelea kulinyonya taifa kwa ufisadi kwa kutumia mifumo ya serikali kufanya mambo kinyume cha sheria.

“Wiki mbili zilizopita, kuna Kampuni kutoka Swaziland imepewa tenda ya kuleta mafuta kutoka nje, wanayoyaita bulk procurement (manunuzi ya pamoja). Tenda ile haikutangazwa, lakini wameongeza bei,” aliendelea.

Alisema ongezeko hilo la bei kwenye tenda hiyo, watu wachache waliotengeneza njama ya tenda hiyo watapata zaidi ya shilingi bilioni 20 ambazo zimesababisha ongezeko la bei ya mafuta lisilo la lazima.

Katika hatua nyingine, Zitto alirusha makombora kwa upande wa Ukawa ambao amedai kuwa wao wamempa nafasi ya kugombea urais, mtu ambaye alitajwa na Chadema kuwa fisadi namba 9 hivyo hawana adhma ya kweli ya kupambana na ufisadi.

Tailor Swift Afunika Tuzo Za MTV/VMAs, Orodha Kamili Ya Washindi Hii Hapa
Sitta Amvaa Lowassa Ufisadi, Ataka Mdahalo Naye Wiki Hii