Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameendelea kushikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio wa halali mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa mwanasiasa huyo, Emmanuel Mvula Zitto alihojiwa na jeshi hilo jana usiku kwa takribani saa moja na baadaye alipelekwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro.

“Jeshi la Polisi wamekataa kumpa dhamana kwa maelezo wanasubiri maelekezo toka kwa wakubwa wao,” ameandika mwanasheria huyo.

Ameongeza kuwa jeshi hilo halikuwapa maelezo ya ziada kama dhamana ya mteja wake iko wazi au la pamoja na masharti ya kupata dhamana hiyo kama ipo.

Imeelezwa kuwa Zitto alikuwa akifanya ziara ya kuwatembelea madiwani wa chama chake katika mikoa nane lakini alishikiliwa kwa kutokuwa na kibali cha kufanya mkusanyiko huo.

Zitto aachiwa huru kwa dhamana ya mamilioni
Aslay na Nandy wapigwa faini milioni 5