Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amempongeza aliyekuwa mshauri wa chama hicho, Profesa Kitila Mkumbo kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Zitto amesema kuwa amepokea barua ya kujiuzulu nafasi ya ushauri wa chama hicho ya Profesa Mkumbo, nafasi ambayo ilikuwa ikimpa sifa za kuhudhuria vikao vya juu vya maamuzi vya chama hicho. Hivyo, amebaki kuwa mwanachama wa kawaida.

Aidha, Zitto amesema kuwa uamuzi wa Rais John Magufuli kumteua Profesa Mkumbo kunaonesha kuwa kuna watu katika vyama vya upinzani ambao ni wazalendo na wanaweza kuaminika.

“Muhimu ni kumsihi Rais ambaye alisema katika Serikali yake hawezi kuteua mtu nje ya CCM kuwa kuna wenye uwezo nje ya CCM,” alisema Zitto.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto ameandika taarifa ndefu kuhusu uteuzi huo. Bofya HAPA kuusoma ujumbe wa Zitto.

TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya kodi
LIVE: Uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki