Mwanamume wa umri wa miaka 38 amekuwa kisa cha kwanza kilichothibitishwa cha virusi vya Covid – 19, nchini Zimbabwe na kuongeza idadi ya maambukizi katika mataifa barani Afrika kufikia 38.

Waziri wa afya nchini Zimbabwe Obadiah Moyo, amesema kuwa mwanamume huyo anayeishi katika eneo maarufu la utalii la Victoria Falls, alikuwa amerejea nchini humo kutoka Uingereza Machi 15.

Mwanamume huyo alijitenga baada ya kuwasili nchini humo na kumuita daktari wake alipojihisi kuwa mgonjwa na baada ya kupimwa, alipatikana kuwa na virusi hivyo.

Waziri huyo amesema kuwa kuwa wizara, inafuatilia watu wote aliokutana nao.

kwa mujibu wa shirika la habari la kimataifa la AP, Bara la Afika limerekodi takribani visa 1000 vya maambukizi ya virusi vya corona na  idadi ya vifo imefikia 17.

Corona yapita na wachezaji tisa FC Sion
Mara: 20 hufariki kila mwaka kwa kichaa cha mbwa