Serikali ya Zimbabwe imesitisha ghafla huduma zote za pesa kwa njia ya simu za mkononi ikisema imechukua hatua hiyo ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu na uhujumu uchumi.

Tangazo hilo lililotolewa na waziri wa habari limepokelewa kwa mshtuko hasa wakati huu wa mwisho wa mwezi ambapo watu wanategemea kupokea mishahara yao kupitia huduma za benki kwa njia ya simu za mkononi.

Serikali hiyo pia imesitisha biashara kwenye soko la hisa la nchi hiyo, ambalo inalilaumu kwa kuendesha shughuli haramu za kifedha.

Zimbabwe ipo kwenye hali mbaya zaidi ya kiuchumi kwa zaidi ya muongo mmoja. Inakabiliwa na ukosefu wa fedha na mahitaji ya misingi ikiwa ni pamoja na mafuta, chakula kikuu ambacho ni unga wa mahindi.

Kulingana na data mpya mfumko wa bei ulifikia karibu asilimia 800 mnamo mwezi Aprili.

Kiongozi wa upinzani aapishwa kuwa Rais mpya Malawi
IMF kuipatia Tanzania fedha kukabili athari za Corona