Msanii wa muziki wa Bolingo na aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka amefunguka na kutoa ushauri kwa aliyewahi kuwa mpenzi na mzazi mwenza wa Naseeb Abdul kuwa afungue mawasiliano yake na Diamond ili aweze kuwasaidia watoto wake.

Asha amepinga vikali hatua zilizochukuliwa na Zarinah Hassan maarufu kama ZariTheBossLady ambaye leo kupitia kurasa wake wa mtandao wa kijamii amelalamikia hatua iliyochukuliwa na Diamond Platinumz ya kusaidia familia 500 kwa kuzilipia kodi ya nyumba huku akidai kuwa Diamond hawahudumii chochote watoto wake.

”Nimuombe Zari kama mwanamke mwenzangu kuweka shutma kwa Naseeb Abdul kwa wakati huu ni dhambi anakosea, sababu mimi kama mzazi kama mwanamke mwenzie hatakiwi yeye kuweka malalamiko hayo kwenye mitandao ya kijamii, Diamond ana familia yake wazazi wake wote wapo hai, kama kuna matatizo asiyatoe katika kipindi hiki cha ramadhani ambacho mtu anataka kujitoa kwa watanzania kwa waliokuwa wengi ambao wameathirika na Corona Virus” amesema Asha Baraka.

Asha amemuomba Zari afungue mawasiliano kati yake na Diamond lakini pia afungue mawasiliano na familia yake nzima.

”Mimi nimshauri afungue mawasiliano kati yake yeye na Diamond, sababu unapumfungia mwanaume mawasiliano atamsaidia vipi, umemblock kila mahali hutaki watoto waje Tanzania, unazuia watoto utapataje msaaada Diamond hawezi kushindwa kulea mpaka watoto 10 katika kipindi hiki”.

Aidha amemtaka Zari amuache Diamond azisaidie familia 500 katika kipindi hiki cha ramadhani ili aweze kupata thawabu kwani familia nyingi zenye uwezo wa chini zimeathirika kufuatia janga hili la corona.

Pia amewashauri Naseeb na Zari kama wazazi wa watoto wawili waondoe tofauti zao na waangalie watoto kwani bifu zao zitawaumiza watoto hivyo ni vyema warudishe uhusiano wao.

Ikulu ya Korea Kusini yatoa tamko kuhusu afya ya Kim Jong-un, ‘yuko hai’
Muhumbili yafunga mashine kusafishia figo Amana

Comments

comments