Mfanyabiashara maarufu ukanda wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan maarufu kama Zarithebosslady, amekula shavu nene mara baada ya kupata dili la kuwa jaji katika mashindano ya ulimbwende nchini Uganda mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Miss Uganda Foundation, Brenda Nanyonjo ambaye amesema shindano hilo la kumtafuta Miss Uganda linatarajiwa kufanyika mnamo Agosti 10, 2018 katika ukumbi wa hoteli ya Kampala

Kupitia mtandao wa Instagram, waandaaji wa shindano hilo wamethibitisha hilo kwa kuandika.

”The Miss Uganda beauty pageant is proud to announce its first patron and judge for #Missug2018 @zarithebosslady . Miss Uganda is a celebration of beauty with a purpose to inspire young women to succeed in life.”

Akimaanisha waandaji hao wanajivunia kumtangaza Zarithebosslady kama mmoja wa majaji watakaoendesha shindano la Miss Uganda 2018.

Aidha shindano la Miss Uganda 2018 limelenga kusherekea urembo na kuhamasisha mafanikio kwa wanawake wenye umri mdogo.

Mbali na kuwa jaji pia Zari ametangazwa kuwa msemaji mkuu katika shughuli zilizoandaliwa na waandaaji wa shindano hilo za  kurudisha fadhila kwa jamii zitakazolenga wasichana wadogo.

 

 

 

EXCLUSIVE: Tazama Kayumba akichambua wimbo wake wa 'mazoea'
Jaji Mutungi avitahadharisha vyama vya siasa