Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe.Hamad Rashid Mohamed amesema serikali imewaweka karantini wananchi 65 wakiwemo vigogo wa serikali na maofisa sita wa afya kwa ajili ya uchunguzi wa virusi vya Corona.

Kwa mujubu wa Radio one strereo Waziri Mohamed amesema lengo la kuwaweka katika karantini  ni kwa ajili ya uchunguzi wa virusi vya Corona.

Hata hivyo ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingiwa na majimaji yenye virusi kutoka mtu mmoja kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Corona  ambao ulianzia nchini China na kusambaa kwa baaadhi ya nchi, ambapo kwa Tanzania mpaka sasa kumekuwa na visa vya wagonjwa 12 wenye maambukizo ya virusi vya hvyo.

 

Avunja ukuta na kuiba kichanga cha wiki mbili
Video : MBOWE waumini wasali nyumbani, MAGUFULI afanya uamuizi mgumu kukabili CORONA

Comments

comments