Kila mwaka zaidi ya watoto 100,000 wanapoteza maisha kutokana na madhara ya migogoro ya kivita, ambayo hupelekea njaa na watoto kukosa misaada ya huduma za kibinadamu.

Shirirka la kimataifa nilaloshughulikia haki za watoto Save the children International, limetoa ripoti hiyo  na kusema kuwa katitka nchi 10 zinazoongoza kwa vita na machafuko jumla ya watoto 550, 000 wamefariki kwenye kipindi cha mwaka 2013 hadi 2017.

Miongoni mwa matatizo ambayo watoto wanakabiliana nayo katika madhara ya vita ni njaa, ukosefu wa huduma za Afya na uharibifu wa miundo mbinu inayokwamisha watoto kupata misaada

Baadhi ya watoto wengine hutishiwa maisha yao, huchukuliwa mateka na kupewa mafunzo ya kijeshi na kuunganishwa katika vita, pia wengine wananyanyaswa kingono, ambapo mtoto mmoja kati ya watano anakumbana na mateso hayo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika hilo unaonesha kuwa mataifa yaliyoathirika zaidi na vita ni Afghanistan, Jamuhuri ya Afrika ya kati, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Iraq, Mali, Nigeria, Somalia, Sudani kusini, Syria na Yemen.

Idadi ya watoto wanao ongezeka katika mauji ya kivita inazidi kuongezeka ni imegeuka kuwa tishio la maisha ya watoto.

 

Video: 21 Savege azungumza aliwekewa mtego kukamatwa
Chadema yatangaza kuanza mikutano ya hadhara

Comments

comments