Kocha Mkuu wa Klabu ya Young Africans, Mbelgiji, Luc Eymael, ameweka wazi kuwa tayari ameshazungumza na mshambuliaji raia wa Ubelgiji, Andréa Fileccia, 28, anaekipiga katika Klabu ya Royal Francs Borains ya nchini Ubelgiji kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo katika kipindi cha Dirisha kubwa la usajili kwa ajili ya kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa, kwa sasa Eymael yuko nchini Ubelgiji ambapo alirejea baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona.

Eymael amesema, tayari ameshafanya mazungumzo na Fileccia na nyota huyo amekubali kutua Young Africans, kilichobaki ni kwa uongozi wa klabu hiyo kumalizana na mchezaji.

“Kwa upande wangu nimeshamaliza mazungumzo na Fileccia na yeye pia amekubali kujiunga na Yanga msimu ujao na hana tatizo lolote katika hilo, lakini kwa sasa kilichobaki ni kwa uongozi wa klabu kumalizana na mchezaji katika masuala binafsi ili dili likamilike”. Alisema Eymael.

Eymael aliongeza kuwa, “Mimi sihusiki kabisa katika mazungumzo ya kifedha, makubaliano ya kifedha ni baina ya klabu na Fileccia”. Alisema Eymael.

Grealish na Havertz wavutana Manchester United
Makonda atangaza oparesheni maalum kukamata wezi Dar "tusilaumiane"