Yanga imeweka rekodi moja ya ajabu msimu huu.. Imesajili wachezaji 22 katika madirisha mawili yaliyopita.. Inashangaza sana..

Unajua kwanini Inashangaza? Nitakwambia..

Pamoja na usajili huo mkubwa, bado hakuna cha maana ilichofanya.. Mpaka sasa IPO katika nafasi ya tatu na ndoto za ubingwa zimeshayeyuka.

Kwanini Yanga walifanya usajili wote huo na bado wakashindwa kufanya vizuri? Ni swali ambalo wanapaswa kujiuliza. Kuna mahali walikosea.

Kwanza, timu haiwezi kufanikiwa kwa kusajili lundo la wachezaji katika msimu mmoja.. Timu inatakiwa kujiimarisha katika maeneo kadhaa tu.. Dirisha baada ya dirisha.

 

 Na ndiyo sababu nataka kuwashauri jambo Yanga.

Wakati usajili ukiwa umekaribia, ni vyema tukalisema hili mapema.. Kwa namna nilivyoitazama Yanga ya msimu huu, wala haihitaji kufanya usajili mkubwa sana mwishoni mwa msimu.

Kwanza kabisa, Yanga inatakiwa kubaki na wachezaji wote muhimu.. Isiwe kama msimu uliopita ambapo nyota walioibeba kama Ibrahim Ajib, Herritier Makambo na Gadiel Michael waliondoka. Wasiruhusu hilo msimu huu.. .

Pili wanahitaji kusajili mastraika wawili wa maana kuja kuziba nafasi ya Yikpe ma Molinga.. Wasifanye kosa katika eneo hili.. Kama atarejea Makambo itakuwa vizuri, walete na straika mwingine wa maana tena.

Pili Yanga wanahitaji winga mmoja wa maana.. Winga ambaye atalingana uwezo na Bernard Morrison au angalau atamkaribia.. Asiwe winga wa kawaida kama Patrick Sibomana..

Kama watasajili Kiungo mmoja mshambuliaji itakuwa vizuri, lakini eneo muhimu zaidi ni beki mmoja wa kati na beki wa kushoto.. Yule Yassin Mustapha wa Polisi Tanzania atawafaa katika upande wa kushoto..

Baada ya hapo Yanga itakuwa imesajili wachezaji muhimu.. Hawapaswi kuzidi sita, vinginevyo itakuwa vurugu.. Wachezaji wengi waliopo Yanga wana uwezo, wanahitaji kuongezewa nguvu tu.

Credit : Gift Macha

Video: Makonda asema watakaokamatwa uzururaji watasafisha mitaro
Waziri mkuu wa Uingereza alazwa akionesha dalili za Corona