Mabingwa Wa soka Tanzania Bara timu ya Yanga wanatarajiwa kurejea jijini Dar Salaam,kutoka mkoani Mbeya ambako iliweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Yanga itarejea jijini na inatarajiwa kuingia kambini moja kwa moja kuendelea na mazoezi kabla ya mtanange wao na Azam FC

iliyopo Visiwani Zanzibar ikijiwinda na mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya tanzania Bara,inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Semptemba 12.

Akizungumza na waandishi wa nhabari Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro, amesema kuwa Yanga inaingia kambini ikiwa tayari imefanya vyema katika kichezo kadhaa ya kirafiki iliyocheza,ambayo imeonyesha mapungufu machache ambayo kocha wa Yanga anaendelea kuyafanyia kazi.

Aidha amesema kuwa kikosi hicho ambacho kimesheni nyota kadhaa mahiri kinaingia kambini kikiwa na lengo la kufanya vyema katika mchezo wake na Azam FC

Chelsea Waongeza Nguvu Safu Ya Ulinzi
Otamendi Huyooooo Man City