Mkali wa Nigeria aliyeyakuna masikio ya mastaa nguli wa Marekani, Wizkid ameeleza jinsi alivyogeuza ujio wa mwanaye wa tatu kuwa siri kubwa kwa wazazi wake.

Akifunguka katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Beat FM, alisema kuwa wazazi wake waligundua amepata mtoto wa tatu kupitia mitandao ya kijamii.

“Kitu cha ajabu ni hiki cha mwisho. Wazazi wangu waligundua nimepata mtoto wa tatu kwa kuangalia mtandaoni,” alisema.

“Mama yangu anataka sasa hivi nijipange nifunge ndoa, nikae na mwanamke mmoja na nizae watoto, lakini mimi nina miaka 27 sasa,” aliongeza.

Msanii huyo mwenye watoto watatu wa kiume ambaye kwake suala la kuwa na mke mmoja bado ni kitendawili alisema kuwa ana mpango wa kuongeza mtoto mmoja na anaomba awe wa kike.

Katika hatua nyingine, Wizkid alieleza kuwa kuna nyimbo mpya ziko jikoni ambazo ni moto wa kuotea mbali. Alisema kati ya nyimbo hizo, ipo aliyomshirikisha rapa wa kike Nicki Minaj.

Dkt Tulia: Sina uhakika kama ‘Mange’ ni binadamu wa kawaida
Maradona amtetea Messi