Uwepo wa madai ya kura kuibiwa kwenye uchaguzi Mkuu 2015, umepelekea Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa kutakiwa kufika mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa ili kuthibitisha madai hayo.

Naibu spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson jana amemtaka Mbunge huyo kufika mbele ya kamati ya maadili ili athibitishe madai yake kuwa kura ziliibiwa kwenye uchaguzi mkuu 2015.

Hayo yamejiri baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu, Jenista Mhagama kuomba mwongozo akidai kuwa iwapo kitendo hicho kilitokea, basi wabunge wote waliopo Bungeni hawapo kihalali.

“Kauli hii inaonesha kuwa uwepo wetu hapa sio halali, jambo ambalo sio sahihi na unavunja kanuni za Bunge, katiba na Sheria” alisema Mhagama.

Pia alimuomba Naibu spika kumtaka Mchungaji Msigwa kufuta kauli yake au kujikita kuzungumza jambo lililokuwa likijadiliwa Bungeni”

Katika majibu yake Msigwa alisema kuwa kura ziliibiwa katika jimbo la kalambo, na alipotakiwa kufuta kauli alisema anaushahidi.

Hatua ambayo ilipelekea Naibu spika kumtaka Mbunge huyo kufika mbele ya kamati ya maadili na Madaraka ya Bunge ili akathibitishe.

China yapika kasi ya 6G
Shiboub aitwa Sudan, Kagere adai kukosa raha