Wizara ya Maliasili na Utalii, imeanza kuyatambua na kuainisha maeneo kwa ajili ya utalii wa Fukwe katika Kisiwa cha Mafia mkoani Pwani kwa ajili ya kuhamasisha Wawekezaji kuchangamkia fursa ya ujenzi wa Hoteli za kitalii.
 
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwaka jana kwa Wizara hiyo kuwa ianzishe Kurugenzi ya Fukwe itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza Fukwe zote nchini.
 
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya siku mbili kisiwani humo ya kutembelea Fukwe pamoja na magofu ya kale, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema kuwa Wizara imejipanga kikamilifu kwa ajili kuwasaidia Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye Fukwe kwa ajili ya utalii.
 
Aidha, katika ziara hiyo, Kanyasu alitembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii vilivyopo kisiwani humo ukiwemo Msitu wa Mlola, Magofu na fukwe katika kijiji cha Kanga pamoja na maeneo ya uwekezaji ya Ras Mlundo Jojo, Banja, Rasini Kanga na Tembo Unyama.
 
Hata hivyo, baada ya ziara hiyo Naibu Waziri huyo alisema kuwa baadhi ya wamiliki wa maeneo hayo ya fukwe yamefanya kuwa mashamba ilihali ni kivutio kikubwa cha utalii ambapo baadhi ya nchi zimekuwa ziikingiza fedha nyingi za kigeni kupitia utalii wa fukwe.
 
  • Video: Ndugai amuita Lissu, asema hana kibali cha kukaa nje ya nchi, Wabunge wa CCM wampongeza CAG
 
  • Faida 6 za mjamzito kushiriki tendo
 
  • Waandishi 38, wanaharakati kukamatwa kwa uchochezi mtandaoni
 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaib Nnunduma alieleza kuwa wilaya yake inawakaribisha Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika wilaya hiyo na kuahidi kuwa atatoa ushirikiano wa kutosha

Ndugai amtumia ujumbe Tundu Lissu, 'Unatakiwa urudi haraka'
Faida 6 za mjamzito kushiriki tendo