Serikali kwa kushirikiana na muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) wamekusudia kushirikishana kwa ukaribu uendelezaji wa sekta ya kilimo ili kuimarisha usalama wa chakula katika kaya zao na nchi kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa kilimo Japhet Hasunga jijini Dodoma Novemba 13, 2019 wakati wa ufunguzi ya mkutano wa semina ya mafunzo ya siku mbili kwa muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) unaomalizika leo.

Bodi mpya TANESCO yatakiwa kufanya kazi kwa weledi

Amesema shughuli hizo zitaongeza kipato na kuboresha maisha ya wanajeshi hao kwa ujumla ikiwemo kuimarisha afya zao kwa kupunguza utegemezi wa ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya kujikimu na maisha baada ya kustaafu.

“Wizara ya Kilimo ipo tayari kushirikiana nanyi katika lengo la kufanya shughuli za kilimo kwa kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na kuwahakikishia upatikanaji wa mbegu bora, mbolea, zana za kisasa za kilimo na viuatilifu,” ameongeza Hasunga.

Wakulima Mtwara wauawa na watu wasiojulikana

Aidha Hasunga amebainisha kuwa kwa kupitia taasisi za serikali na mamlaka zilizopo wizara imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa pembejeo kwa ujumla kutokana na umuhimu wake kwa kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa Taifa.

Hata hivyo Waziri Hasunga amewahimiza wanajeshi hao na wakulima wote nchini kuzingatia matumizi bora ya pembejeo na kufuata ushauri wa kitaalamu kwani itawasaidia kuongeza faida katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na kujiongezea kipato.

Bunge lapitisha wanaoambukizwa Ukimwi kulipwa fidia

“Sekta ya kilimo inachangia asilimia 28.7 ya pato la Taifa, asilimia 65.5 ya ajira, asilimia 65 ya malighafi ya viwanda na asilimia 30 ya mapato ya nje hivyo uzingatiaji wa matumizi bora ya pembejeo na kufuata ushauri wa kitaalamu utasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo,” amesisitiza Hasunga.

Hata hivyo amesema programu ya Kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ili kuweza kuchangia kwa ufanisi ukuaji wa uchumi wa nchi na kutekeleza vipaumbele vya Taifa.

Aidha Hasunga amefafanua kuwa jitihada za serikali zinalenga kuondoa vikwazo na changamoto za ukuaji wa sekta hiyo na kuimarisha mapato ya kilimo, kuboresha ukuaji wa mapato ya wakulima wadogo, kujitosheleza kwa chakula, uongezaji thamani ya mazao, ajira na kufikia nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Watanzania mbioni kujipima Ukimwi kwa mate

“Sasa MUWAWATA wanapaswa kufanya wasilisho la shughuli za kilimo wanazozifanya na zile wanazotarajia kufanya kubainisha changamoto walizonazo na mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto hizo ili kifikia malengo tunayojiwekea,” amebainisha Hasunga.

Mkutano huo unaomalizika hii leo unalenga kuwashirikisha wadau fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo ili kuongeza mchango wake katika pato la Taifa ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya wakulima wadogo.

Sambamba na hatua hiyo pia washiriki wataongeza ufahamu wa fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo, kuunganishwa na wadau wawezeshaji na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na sekta binafsi kutoa maoni, ufafanuzi na kuwashauri MUWAWATA namna ya kushiriki katika kilimo.

Zlatan Ibrahimovic amalizana na LA Galaxy
Bodi mpya TANESCO yatakiwa kufanya kazi kwa weledi