Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa imeanza kupiga kura ya maoni ya siri katika vijiji vyote vya tarafa tano za wilaya hiyo ili kuwabaini waharifu wa matukio ya ubakaji na ulawiti ambayo yanaonekana kukithiri katika wilaya hiyo na kuifanya wilaya hiyo kuwa ya kwanza kati ya wilaya tatu za mkoa huo kwa ukatili huo.

Hayo yamesemwa na Kaimu katibu tawala wa wilaya ya Mufindi, Joseph Mchina ambapo amesema kuwa kura ya siri ya maoni imeanza tangu Januari mwaka huu katika vijiji na mitaa na baadaye itafanyika katika taasisi za elimu zikiwemo Shule za Sekondari, Msingi na vyuo ili kuwabaini watu wanaohusika na matukio hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Makoga amesema kuwa sababu za matukio ya kikatili ya ubakaji na ulawiti katika mkoa wa Iringa zinachagizwa na imani za kishirikina mambo ambayo yanatokana na ukosefu wa elimu.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliozungumza na Dar24 Media wamesema kuwa utaratibu wa serikali kupiga kura ya maoni ya siri uende sambamba na uandaaji wa takwimu sahihi kwa kuwa bado kunataarifa zilizipo hazina uhalisia na matukio.

Viongozi wa Dini nchini waaswa kuliombea Taifa na Rais Magufuli
Video: Tandale yawa Fursa, Biashara kwa Vijana