Klabu ya West Bromwich Albion imeingai kwenye harakati za kumuwania beki wa pembeni wa Chelsea Branislav Ivanovic.

Ivanovic anaamini mchezo wa kombe la FA dhidi ya Brentford uliochezwa siku ya jumamosi ya juma lililopita, ulikua wa mwisho kwake ndani ya klabu ya Chelsea, na kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka klabuni hapo kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa.

West Bromwich Albion wameingia kwenye mpango wa kumsajili Ivanovic wakitambua tayari kuna klabu kama Zenit St. Petersburg ya nchini Urusi imeshatuma ofa ya kutaka kumsajili beki huyo kutoka nchini Serbia.

Hata hivyo mpango wa West Bromwich Albion, unatajwa kuushtua umma wa mashabiki wa soka nchini England, ambapo mapema hii leo, kituo cha televicheni cha Sky Sports kimeripoti kuwa, usajili wa Ivanovich ndani ya klabu hiyo unapewa kipaumbele na meneja Tony Pulis.

Hata hivyo maamuzi ya beki huyo mwenye umri wa miaka 32, ndio yatakua chachu ya kufahamu ni wapi atakapoamua kucheza soka lake baada ya kuondoka Stamford Bridge, ambapo amedumu kwa kipindi cha miaka minane.

Mpaka sasa Ivanovic ambaye alisajiliwa na Chelsea akitokea Lokomotiv Moscow, ameshacheza michezo 261 akiwa na The Blues na kufunga mabao 22.

#HapoKale
Mourinho Aigwaya PL, Ageukia EFL Cup, FA Cup