Wenyeviti 50 wa Serikali za Mitaa wa Chama cha Wananchi (CUF) jijini Dar es salaam wametangaza kuunga mkono hatua zilizochuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la upande wa Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba kuwavua uanachama wabunge wanane wa viti maalum na madiwani wawili.

Wakiwakilisha wenzao 36, wenyeviti 14 kutoka mitaa mbalimbali ya halmashauri za manispaa tano za jiji la Dar es salaam, wamesema kuwa wamefikia hatua hiyo mara baada ya kujirisha na kazi nzuri inayofanywa na Prof. Lipumba.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake 14 mbele ya waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Keko Mwanga B, Shilingi Shilingi amesema kuwa wanaunga mkono uamuzi wote wa Baraza Kuu la Uongozi kwani wabunge hao walikuwa wakikihujumu chama.

“Tunatambua kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ni kama katibu mkuu lakini kwa sasa nafasi yake ina kaimiwa na Magdalena Sakaya kutokana na yeye kutotekeleza vizuri majukumu yake kwa mujibu wa sheria na katiba ya CUF,” amesema Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Keko Mwanga B, Shilingi Shilingi

Hata hivyo, Shilingi amewataka watu wanaoingilia mgogoro wa CUF kuacha mara moja na kwamba suala hilo ni la kikatiba na kwamba tayari liko mahakamani na muda si mrefu uamuzi utatolewa.

 

Usajili 2017/18 Wakamilika, Kanuni Zashusha Timu Mbili
DAWASCO yaja na mfumo mpya kwa wateja wao