Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefafanua sababu ya kuwazuia waandishi wa habari kufanya mahojiano na wabunge wa upinzani kwa kusema wabunge hao wamekuwa na utaratibu wa kutoka nje mara kwa mara.

Ndugai ametoa ufafanuzi huo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kauli yake aliyoitoa ya kuwazuia waandishi wa habari kufanya mahojiano na wabunge wa upinzani ambao waliamua kutoka nje ya Bunge baada Mbunge Arusha Mjini kusimamishwa mikutano 3 ya Bunge.

“Hatukusema sasa waandishi msiwe mnaongea na wabunge huko nje, lakini waandishi mkiacha kuwafuatilia wataacha wakitoka saa saba si Bunge limeahirishwa wakasema wanayotaka, wakitoka wanaleta mtafaruku na kusababisha mijadala muhimu ya ndani ya Bunge isiwe na waandishi.” amesema Spika Ndugai

Aidha, kuhusiana na hatma ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Ndugai amesema kuwa kuna watu wana madeni makubwa zaidi ya hayo lakini hawaja changanyikiwa kama Lema, lakini akasema muda ujao, awepo asiwepo hawataruhusu tena bunge kudhamini wabunge kuingia kwenye madeni makubwa.

Amesema kuwa wanaotetea lazima watetee kwa sababu hawajui hali halisi ni nini, lakini mwisho wa siku hela yao ndiyo inayotumika,huku akitolea mfano kwa wale waliotimuliwa nane (wabunge wa CUF) wanadaiwa zaidi ya bilioni 1 na hawana uwezo wowote wa kulipa.

Hata hivyo, April 2, 2019 Kamati ya Maadili, ilitangaza kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad na kutangaza kumsimamisha mikutano miwili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

  • Aliyewatapeli mahujaji mwaka 2017 anusurika kichapo
  • Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 2 mkoani Njombe
  • Wahamiaji 12 wakamatwa mkoani Njombe

 

Video: Bunge labariki msajiri kuvishughulikia vyama, JPM akerwa na Wizara ya Maji
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Aprili 6, 2019

Comments

comments