Muigizaji wa filamu bongo na Afrika Mashariki, Wema Sepetu, amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameletwa duniani na Mungu kwa lengo la kusaidia watu na si vinginevyo.

Ameyasema hayo mara baada ya Makonda kuonyesha nia ya kumsaidia kumsafirisha kijana Ahmed Albaity kwenda nchini China kwa lengo la kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa aliokuwa nao wa kupooza mwili mzima.

“Nikisema ‘RC’ wangu ni mtumishi wa Mungu basi namaanisha, mimi ‘sometimes’ nasema uliletwa duniani kuja kufanya ya Mola wako tu. Mungu azidi kukubariki ‘my RC you are just like a guardian angel’, ipo siku wataelewa tu. ‘I got a Good Feeling about Ahmed and Inshallah God will work a miracle, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho,”amesema Wema Sepetu.

Hata hivyo, Kijana Ahmed Albaity alipooza mwili wake mnamo 2007 baada ya kucheza vibaya michezo ya kujirusha ‘dive’ katika bahari na kwa bahati mbaya alikosea na kujipiga kichwa chini ambapo ilipelekea kupata matatizo yote hayo mpaka sasa.

Mwanafunzi wa Kitanzania auawa kikatili Afrika Kusini
Apewa likizo ya lazima baada ya mgonjwa kufanyiwa operesheni ya ubongo kimakosa