Uongozi wa WCB pamoja na Wasafi Media kwa pamoja wamezindua rasmi Tamasha la Wasafi Festival 2019 linalotarajiwa kuanza Julai 12 mwaka huu na kuwashukuru BASATA kwa kuwapa kibali mara nyingine kufanya tamasha hilo

“Napenda Kutangaza rasmi kuwa Wasafi Festival 2019 nimeizindua na mkoa wa kwanza ambao tunaenda kuwasha moto wa burudani ni pande za Mulba na shoo itapigwa pale tarehe 12 mwezi wa saba’ amesema Diamond Platinumz

Ambapo Diamond Platinumz ametaja sehemu tatu ambazo wanatarajiwa kuanza nayo ambapo ni Muleba, Tabora na Iringa.

Ambapo Muleba wanatarajia kufanya tamasha hilo mnamo Julai 12, Tabora mjini Litafanyika Tarehe 14, julai na Iringa kufanyika tarehe 20 Julai mwaka huu 2019.

“Tukimaliza tu Muleba, tunapunzika siku moja, kisha tarehe 14 tunaingia mkoa wa Tabora kuwasha moto pale. Na niwaambie tu mimi binafsi nimejipanga kisawasawa, na sina utani jukwaani” amesema.

Aidha Babu Tale ambaye ni kiongozi wa Wasafi Festival amesema mwaka jana walifanya mikoa michache ila mwaka huu wanatarajia kufanya mikoa mingi zaidi kuanzia nane hadi kumi hivyo amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kutazama shoo zao.

Diamond ameongezea kuwa msimu huu watafanya tamasha hilo tofauti sana na ambavyo limekuwa likifanyika.

 

 

 

Siasa yatajwa kuvuruga mikopo ya SIDO, mali za wadaiwa sugu kutaifishwa
LIVE: Yanayojiri bungeni jijini Dodoma

Comments

comments