Uongozi wa lebo ya WBC inayomilikiwa na Diamond Platinumz imemfungulia milango yote aliyekuwa mwanafamilia wa kundi hilo, Rich Mavoko kushiriki tamasha la Wasafi Festival, wakieleza pia nia ya kumuwahi yeye na wasanii wengine mwakani.

Meneja wa WCB, Babu Tale wiki hii amesema kuwa Mavoko anaweza kuwa kati ya wasanii watakaopanda kwenye jukwaa la tamasha hilo lakini wanapata changamoto ndogo kwa mwaka huu.

Akielezea changamoto hiyo, Babu Tale ameeleza kuwa mikoa mingi ambayo wanapita hivi sasa, ni mikoa ambayo msanii huyo ameshapita akiwa na tamasha la Fiesta hivi karibuni, hivyo wakifanikiwa kumpata mapema mwakani watamuweka kwenye ratiba mbele ya washindani wao.

“Kwanini Rich Mavoko asipande? Kwa sababu ya muda na mikoa yote tunayoenda yeye ameshaenda [hivi karibuni] kwahiyo hatukuweza kumuwahi. Let’s say Inshallah mwaka unapoanza tutakuwa na nafasi kubwa ya mikoa zaidi ya 15 hadi 20, na wote ambao hawapo mwaka huu [akiwemo Mavoko], na sisi tutawawahi tuwe nao wote. Hii ni yetu sote,” Babu Tale anakaririwa na SamMisago.

Kwa mujibu wa TCRA, Diamond Platibumz ni mmoja kati ya wamiliki wa Wasafi TV ambao ni waandaaji wa tamashala Wasafi Festival, akiwa na asilimia 43 za hisa.

Rich Mavoko aliachana na WCB kutokana na mgogoro wa kimkataba na hivi karibuni ameshiriki tamasha la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Media Group, katika mikoa zaidi ya 10 nchini.

Clouds Media Group na Wasafi waliingia katika ushindani uliogeuka kuwa uhasimu wa kibiashara unaohusisha team mbili za menejimenti ya makampuni hayo ambayo yote yanamilikiwa na ‘Familia ya Joseph Kusaga’.

Zitto atumia ‘bata’ kushawishi Urais 2020
Wababe Deontay Wilder, Tyson Fury kuitikisa dunia leo

Comments

comments