Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ametangaza rasmi ujio wa tamasha lao kubwa litakalojulikana kama Wasafi Festival ambalo linatarajiwa kufanyika ndani ya mwaka huu.

Bado haijawekwa wazi wapi na lini hasa tamasha hilo litafanyika, Diamond ametumia ukurasa wake wa Instagram kuujuza umma na mashabiki wa Wasafi Classic ujio wa tamasha hilo.

“Kama Naiona hiyo #WasafiFestival Huu Mwaka Sijui hata tuanzie Mkoa gani????‍♂️,” ameandika Diamond Platinumz.

Hata hivyo Disemba 2016, WCB walifanya matamasha makubwa likiwemo la Wasafi Beach Party lililofanyika Jangwani Sea Breezy jijini Dar es Salaam, na jingine mkoani Iringa.

Diamond Platinumz ni moja kati ya wasanii wachache waliowahi kutokea nchini kwa ubunifu wake na kukuza vipaji vya wasanii wengine na kufanya vijana wengi watake au waupende kufanya Muziki.

WCB likiongozwa na rais wao Diamond Platinumz wasanii wengine ni Harmonize, Rich Mavoko, Lavalava, Marombosso, RayVany na Quen Darleen.

Taarifa juu ya tamasha hilo tutaendelea kukujuza hapa hapa Dar24, ili kujua ni wasanii gani watapa nafasi ya kushiriki kutumbuiza katika tamasha hilo linalotarajiwa kuwa tamasha kubwa.

 

Rais RT ampongeza Mkurugenzi mpya MultiChoice
Afya ya Jet Li yawa tete, ageuka mzee ghafla