Kutokana na sakata la ufisadi wa fedha za ujenzi wa mabwawa nchini Kenya, Waziri wa fedha , Henry Rotich, amejisalimisha kwa maafisa wa upelelezi leo muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa mashtaka wa nchi hiyo kuagizwa akamatwe.

Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari nchini kenya, waziri Rotich alipelekwa kwa gari hadi katika makao makuu ya idara ya upelelezi ambako anahojiwa kuhusu malipo yaliyotolewa kwa ujenzi wa mabwawa mawilini nchini humo.

Anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliyopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwaajili ya ujenzi wa mabwawa.

Hapo awali Mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya Noordin Haji amekuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kumshtaki waziri wa fedha na maafisa wengine wa Serikali ya nchi hiyo juu ya ufisadi uliojitokeza kwenye ujenzi wa mabwawa.

Haji ameeleza kuwa watashtakiwa kwa kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi.

“Imebainika kwamba namna mpango ulivyoidhinishwa, ulivyo patikana na malipo yalivyotolewa kwa mradi wa mabawa hayo, umegubikwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria” aliongeza Haji

Hata hivyo mnamo mwezi machi Waziri Rorich kupitia tangazo kubwa kwenye gazeti nchini humo, alikana kuhusika na tuhuma hizo, pia kampuni hiyo ya Italia CMC de Ravenna pia imejitokeza na kukana hadharani tuhuma hizo.

Maafisa wengine walioagizwa kukamatwa kushtakiwa ni pamoja na katibu mkuu katika wizara ya fedha kamau Thugge, Dkt Susan Jemutai Koech kutoka wizara ya jumuiya ya Afrika Mashariki na mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya maendeleo ya Kerio Valley (KVDA) David Kimosop.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 23, 2019
Rais Magufuli ampa Bashe mtihani, amkumbusha ‘machachali’ ya bungeni