Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa yeye ni miongoni mwa wazazi ambao wamekuwa wakiwakagua watoto wao mara kwa mara ili kujua kama wamefanyiwa vitendo vya ukatili.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati wa muendelezo wa vikao vya Bunge ambapo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Rombo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo, Joseph Selasini ambaye alihoji juu ya wazazi kupewa elimu ya kuzungumza na watoto wao.

”Wazazi tutimize wajibu wetu kwa watoto, mimi namkaguaga binti yangu, lazima tuwakague hawa watoto wa miaka 3 walau muogeshe utajua anachangamoto gani, tukiwa bize kutafuta hela watoto wanaharibika, mtoto analawitiwa miezi 3 mzazi hajui.”amesema Ummy Mwalimu

Aidha, ameongeza kuwa Mwananchi yeyote ambaye ana taarifa kuhusiana na ukatili wa mtoto apige simu 116 na itapokelewa na taarifa itafika kwenye vyombo vya Serikali, na itafanyiwa kazi, huku akisema wameanzisha madawati ya jinsia kwenye Jeshi la Polisi yapo madawati zaidi ya 350.

Kwasasa Bunge linaendelea jijini Dodoma ambapo mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio ya bajeti zao kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Waziri Mkuu wa Uingereza atangaza kujiuzulu
Simba yafanya maandalizi ya kukabidhiwa kombe