Hatimaye matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni ya nafasi ya ubunge katika majimbo ya Tarime Mjini na Tarime vijijini yametangazwa baada zoezi la upigaji kura kuahirishwa mara mbili kufuatia tuhuma za hujuma.

Matokeo hayo yameleta taswira tofauti  baada ya kumuangusha Waziri wa Kazi Na Ajira, Bi. Gaudencia Kabaka akishindwa katika kinyang’anyiro cha kuwania kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Tarime Mjini, nafasi iliyochukuliwa na Michael Kimbaki aliyepata kura 3908 dhidi ya wagombea wanzake watano akiwemo waziri huyo.

Kwa upade wa jimbo la Tarime Vijijini, Christopher Kangoi alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 15928 na kuwashinda wagombea wenzake saba akiwemo mbunge mbunge anaemalizia muda wake, Nyambari Nyang’wine.

Akizungumza baada ya kutangazwa matokeo hayo, Nyambari Nyang’wine alidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na mizengwe na haukuwa huru kama ilivyotarajiwa. Hivyo, hakubaliani na matokeo hayo.

Kwa upande wake Bi. Gaudencia Kabaka alionekana kukubaliana na matokeo hayo na kuwashukuru wanachama wa chama hicho waliompigia kura.

gaudencia

Awali, Bi. Gaudencia Kabaka na Nyambari Nyang’wine walituhumiwa kuhujumu mchakato wa uchaguzi huo baada ya kupatikana makaratasi ‘fake’ kwenye masanduku ya kupigia kura yakiwa na alama za vyema kwenye majina ya wagombea hao. Wagombea hao walipinga vikali tuhuma hizo na kudai kuwa hawakupewa nafasi ya kusikilizwa ili kujibu tuhuma hizo kabla ya kuahirisha zoezi la uchaguzi hapo awali.

Bi. Gaudencia Kabaka anakuwa waziri wa sita wa serikali ya awamu ya nne kushindwa katika kura za maoni hivyo ndoto zao za kurejea bungeni zimezima.

Maywether Kumalizia Ndondi Mwezi Septemba
Arsenal Kumkosa Wilshere Kwa Majuma Kadhaa