Waziri Mkuu wa Fiji, Frank Bainimarama, amemtembelea Rais wa Kenya, Uhuru kenyatta alipohudhuria mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi jijini Nairobi.

Bainimarama ambaye ni mwanamume, alikuwa amevaa suti ya sketi na viatu vya wazi wakati alipopata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa makazi nafuu katika eneo la Ngara jijini Nairobi.

Jambo hilo limewashangaza wengi huku kwenye mitandao ya kijamii wakionyesha kupigwa na butwaa na vazi alilovaa Waziri mkuu huyo, ambalo ni maarufu kwa wanaume wa Fiji likifahamika kwa jina la ‘Suti ya Sulu’.

Aidha, Sulu ya wanawake hufahamika kama Sulu-i-ra. Suti ya Sulu inachukuliwa kama vazi la kitaifa la Fiji na huangaliwa kama utambulisho wa jamii ya Wafiji. Vazi hilo ambalo huwa wakati mwingine sketi yake inakatwa katwa upande wa chini huvaliwa na wanaume na wanawake wa Fiji.

Sulu zilivaliwa na watu wa Fiji tangu enzi za ukoloni katika karne ya kumi na tisa na mwanzo zililetwa na wamisionari waliokuwa wakitoka Tonga na katika kipindi hiki sketi hizo zilikuwa zikivaliwa na Wafiji kuonyesha kuwa wamejiunga na Ukristo.

Hata hivyo, Sulu za wanawake zinazovaliwa kila siku hufahamika kama sulu-i-ra, na Sulu ndefu wanazovaa rasmi au wakati wa matukio ya sherehe hufahamika kama sulu jaba.

DC aagiza kila mwananchi kudhibiti mimba kwa wanafunzi
Video: Balaa lingine mifuko ya 'rambo' lafichuka, Profesa Kabudi aeleza nchi inavyolindwa