Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Dodoma wajitokeze kwa wingi kuchangia damu ili iweze kutumika kuokoa maisha ya wengine.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwl. Nyerere, jjini humo.

Amesema kuwa Serikali inaendelea na kampeni ya kuhakikisha vituo vya afya na hospitali vinakuwa na akiba ya kutosha ya damu kwa ajili ya wagonjwa wenye kuhitaji damu.

“Tunawasihi Watanzania waende kuchangia damu ili benki ya damu iwe na akiba ya kutosha endapo mtu ataenda pale kufanyiwa upasuaji na akapoteza damu nyingi, au awe amepata ajali au ameenda kujifungua, apate damu kwa haraka kutoka kwenye benki yetu,”amesema Majaliwa

Aidha, akizungumzia kuhusu upimaji wa virusi vya UKIMWI (VVU), Waziri Mkuu amesema kampeni inafanyika lakini kasoro iliyopo ni kwamba wanaojitokeza kwa wingi kupima afya zao ni wanawake na wanaume hawapimi.

“Mimi ndiye balozi wenu akinababa kwenye kampebi ya kitaifa ya upimaji VVU. Nataka niwahimize twende leo tukapime, tusitegemee matokeo ya vipimo vya mke. Wengi mnasubiri matokeo ya mke, akisharudi kutoka kupima na kusema niko safi, basi na wewe unaanza kufurahi unasema niko safi, hapana!ameongeza Majaliwa”

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama Mkoa wa Dodoma, Dkt. Leah Kitundya alimweleza Waziri Mkuu kwamba Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ina upungufu wa damu kwa sababu kuna matukio mengi yanayosababisha upungufu wa damu,

“Tukisema kuwa tunakusanya chupa za kutosha, tunahitaji tuwe na chupa 1,000 hadi 1,500 za damu lakini katika hali ya kawaida huwa tunakusanya chupa za damu 850 hadi 950 tu,” amesema.

CAG mstaafu awashauri wasioridhishwa na CAG Assad
Muongozaji wa filamu John Singleton afariki Dunia