Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemtaka katibu mkuu wa wizara ya Biashara na viwanda Zanzibar, Juma Hassan Reli, kuzuia utoaji wa vibali vya kuingiza sukari kutoka nje hadi pale inayozalishwa na kiwanda cha Zanzibar itakapo isha.

Majaliwa ametoa agizo hilo jana, alipotembelea kiwanda cha kuzalisha sukari cha Zanzibar kilichopo eneo la Mahonda, wilaya ya kaskazini A mkoa wa kaskazini Unguja.

Amesema haiwezekani kiwanda hicho pekee kinachozalisha tani 6,000 za sukari kwa mwaka kikakosa wateja wakati mahitaji ya zanzibar ni tani 36,000 kwa mwaka.

Amesisitiza kuwa ni vizuri wizara ikahakikisha sukari inayozalishwa na kiwanda hicho inapewa kipaombele cha kwanza kununuliwa, kwa sababu wanauhakika na ubora wake kwakuwa wameshuhudia uzalishaji wake kuanzia hatua ya kwanza ya awali miwa ikiwa shambani.

Majaliwa amesema Serikali imeamua kukuza uchumi kwa kupitia sekta ya viwanda, hivyo nilazima viwanda vya ndani vikalindwa.

“Viwanda vinasaidia katika kuondoa tatizo la ajira, vinawapa wakulima soko la uhakika la mazao yao pamoja na Serikali kupata kodi ya uhakika” amesema Majaliwa.

Awali Mkurugenzi mkazi wa kiwanda hicho, Rahim Bhaloo alisema kiwanda chao kinazalisha tani 6,000 kwa mwaka huku kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani zaidi ya 20,000 ila tatizo ni soko pamoja na ardhi ya kutosha kulima miwa.

Alisema kutokana na uhaba wa soko, sukari waliyozalisha msimu wa mwaka 2019/20 wameuza tani 2,800 tu na kiasi cha tani 3,200 bado kipo kiwandani hapo, hivyo aliiomba Serikali iwasaidie kuwatafutia masoko na ardhi ili waweze kuongeza uzalishaji.

Naye katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Zanzibar, alimhakikishia Waziri mkuu kwamba sukari yote iliyopo kiwandani hapo itakuwa imesha nunuliwa ifikapo mwezi Februali mwaka huu na maelekezo kuhusu utoaji wa vibali vya uingizaji sukari yatafanyiwa kazi.

Fanya haya kulinda meno ya watoto kutoboka, kuoza
Rukwa: Walimu wenye mahusiano na wanafunzi kupigiwa kura za siri